Back to Top

Kiswahili and Other Foreign Languages

WALIMU

1. IKHALACHI VITALIS PETER - MKUU WA IDARA
2. SAI JANE -MKUU WA SOMO: KISWAHILI
3. ONGERI NIMROD
4. MUSI DAVID
5. TSUMA BEAUTTAH
6. OWOLLA JANET
7. KAMADI DAVID
8. ALIELO RUTH ASIKOYE
9. SIMWA PETER MUYEKU
10. NYONGESA EVERLYNE
11. BARSIGAN FELIX – HEAD OF SUBJECT: GERMAN
12. AMBANI CLAYTON -HEAD OF SUBJECT: FRENCH

KUTUHUSU

Idara ina baadhi ya walimu wenye tajriba kubwa katika ufunzaji na ujifunzaji wa lugha. Katika Kiswahili kuna vigogo waliofunza kwa takriban miaka thelathini na kuna chipukizi. Mchanganyiko huu ni mzuri kwa ajili ya nguvu walizonazo chipukizi na uzoefu wa vigogo. Kazi inaendelea vilivyo.

Matokeo ya Kiswahili yanazidi kushamiri kila kukicha na somo la Kiswahili ni miongoni mwa masomo pendwa. Mwaka 2015, tulitimu kiwango cha 11.4.
Tuawahimiza wanafunzi kukisema Kiswahili kwa ufasaha huku wakizingatia hoja na uadilifu. Ni jukumu letu sote kuhakikisha hili linaafikiwa ili kufikia malengo ya jamii nzima ya elimu ya taifa katika shule za sekondari. Ingawa hivyo, kuna changamoto chungu nzima hususa kutoka kwa wanafunzi walio na mitazama hasi juu ya Kiswahili. Baadhi yao maandalizi katika shule za msingi hayakuwafikisha kwa viwango vitarajiwa.

Vitabu vya kiada na ziada vipo. Kwa hakika tunawashirikisha pakubwa katika kutafiti maarifa wenyewe kwa wenyewe. Hili linawezekana tu pale ambapo kuna nyenzo za kutosha. Kwa sasa tunahimiza kila mwanafunzi kuwa na nakala ya Darubini ya Sarufi chake Assumpta Matei ili kujisomea. Hali hii imerahisisha sana mafunzo ya sarufi ambayo kwa mujibu wa mtaala yameegemezwa katika isimu. Tamthilia na riwaya zilizotathminiwa miaka iliyotangulia huwashughulisha sana wanafunzi wa vidato vya 1 na 2. Insha husistizwa toka viwango vya chini kufikia viwango vya juu huku wakihimizwa kuwa wabunifu zaidi.
Darasani matumzi ya tarakilishi yamewaongeza wanafunzi utashi wa kujifunza. Kwa hakika mbinu hii ya kielektronik imerahisisha kazi kwa wakufunzi na kuwafanya waelekezi tu.

KIJERUMANI

Mwalimu Barsigan ametwika zigo la kupigia debe Kijerumani na kuhahakikisha kuwa wanafunzi wanaking’amua kwa muda mfupi wanaotangamana naye. Ukweli ni kuwa Barsigan analitekeleza jukumu hilo na hatuna wasiwasi. Wanafunzi wanachangamkia somo hili. Wanashiriki katikaTamasha za Muziki na tayari dalili ni nzuri mno. Tamaa yetu ni kuwaona hawa wanafunzi wakijipenyeza katika nafasi mbalimbali kule Ujerumani kwa kuendeleza kisomo chao au hata kufanya biashara au kazi zingine.
Nyenzo za kufunzia Kijurumani bado hazitoshi na tunajaribu kuwaomba wahisani kutukomoa.

KIFARANSA

Kifaransa hakijashamiri kiasi cha kuridhisha hapa shuleni. Matumaini yetu ni kuwaona wanafunzi wengi wakikichangamkia na kufanya mitihani ya kitaifa. Ukweli ni kuwa Kifaransa kina changamoto chungu nzima. Kila walimu tunaopata hushindwa kukikwamua katika lindi hili. Kwa vile somo hili halifanywi vyema katika mitihani ya kitaifa, linahofisha wanafunzi kulichukua kwani ni kama kujitia kitanzi. Tunafanya juu chini somo hili lisiondolewe katika ratiba ya mafunzo kwa kuwapa wanafunzi fursa za kuzuru shule zifanyazo vizuri katika Kifaransa na kumhudhurisha mwalimu warsha na makongamano ya walimu wa Kifaransa angaa tuone mabadiliko. Kifaransa kama lugha ni muhimu sana kwa vile ni miongoni mwa lugha sifika za kimataifa na hutumiwa na nchi nyingi sana barani Afrika. Mwalimu Ambani Clayton kwa sasa usukani ni wake na twamhimiza kwamba yawezekana kubadili mambo.

Washirika wetu wa karibu ni wengi. St Joseph’s Rapogi, Kisumu Girls, St Mary’s Yala, Sacred Heart Mukumu, Kakamega High School, Homa Bay High School, Kapsabet Girls na Kipsigis Girls. Tuna ukuruba na Sunshine High School, Mary Hill Girls na Starehe Boys Centre.hali kadhalika St Mary’s Girls Mumias na Butere Girls. Tunahusiana kwa vizuri zaidi na majirani zetu Keveye Girls, Moi Girls Vokoli na Igunga Girls.

Mtu ni watu.

Wasalamu.
Mudiri.